Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo Amanda kuinunua Spurs

T6WNVSGEIYDCX4OM6XQOW3OFQA Mrembo mwenye pesa ndefu, Amanda Staveley

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mrembo mwenye pesa ndefu, Amanda Staveley ameripotiwa kuwa na mpango wa kununua hisa kwenye klabu ya Tottenham Hotspur.

Ripoti zinadai, mmiliki mwenza huyo wa zamani wa Newcastle United ana pesa za kutosha kutoka kwa washirika wake wa Mashariki ya Kati pamoja na utajiri wake mwenyewe ndiyo maana anataka kuwa kwenye orodha ya wamiliki wa klabu ya Spurs.

Mrembo Amanda, 51, alinunua hisa zake kwenye klabu ya Newcastle mwaka 2021, lakini aliachana na timu Julai mwaka huu. Na sasa ana pesa za kutosha kwa ajili ya kuwekeza kwenye timu nyingine, huku matumaini yake makubwa ni kununua hisa kwenye klabu ya Spurs.

Na washirika wake baada ya hapo wanaweza kuongeza hisa zaidi kwenye klabu hiyo ya London.

ENIC, kampuni inayomiliki hisa nyingi kwenye klabu hiyo, ambayo inamilikiwa na familia ya bilionea Joe Lewis na mwenyekiti wa klabu, Daniel Levy, ambaye pia ana hisa zake, wameweka wazi milango ya kupiga bei baadhi ya hisa kwa wawekezaji wengine.

Tottenham inathaminishwa kuwa na thamani ya Pauni 2.42 bilioni kwa mujibu wa Forbes.

Hivyo, dili la kumiliki asilimia 25 za hisa kwenye klabu hiyo zinaweza kumgharimu mrembo Amanda, Pauni 650 milioni.

Spurs imefungua milango ya wawekezaji wapya na jambo hilo halitamhitaji mrembo Amanda kuuza hisa zake chache kwenye klabu ya Newcastle. Kampuni yake inayomiliki hisa huko St James’ Park zipo chini ya asilimia 9.9 ambazo ndiyo kikomo kwa mtu mmoja kumiliki timu mbili.

Mrembo Amanda alisema mwezi uliopita: “Sitaki kuipoteza Newcastle.”

Amanda alisaidia uuzwaji wa klabu ya Man City kwa Pauni 210 milioni mwaka 2008.

Chanzo: Mwanaspoti