Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpole azidi kutisha Geita Gold ikitinga nafasi ya tatu

George Mpole Goli 15 Wachezaji wa Geita Gold wakishangilia goli la Mpole

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuzuiwa kwa takribani dakika 78 hatimaye George Mpole ameibuka na kuonyesha kuwa hakamatiki akiifungia timu yake bao la pili ambalo limeihakikishia ushindi muhimu timu yake na kutinga nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Geita Gold imeibuka leo na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi ambao umechezwa saa 10 jioni katika Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita.

Matajiri hao wa Dhahabu wamepata bao la kwanza mapema tu mnamo dakika ya 8 likifungwa na Raymond Masota akimalizia mpira wa faulo uliopigwa na George kisha ukatemwa na kipa wa Dodoma Jiji, Hussein Masalanga.

Bao hilo limedumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza na kuipeleka Geita Gold mapumziko ikiwa kifua mbele huku ikitengeneza nafasi kadhaa za mabao ikiwemo ya dakika ya 27 ambapo shuti la Raymond Masota limegonga nguzo na kurejea uwanjani.

Kipindi cha pili Dodoma Jiji imekuja juu ikitawala mchezo na kuwadhibiti wenyeji wao ambao hawakutengeneza nafasi nyingi huku wakifanya juu chini kulinda bao lao.

Lakini dakika ya 78 George Mpole akaibuka na kuiandikia timu yake bao la pili na la ushindi kwa juhudi binafsi baada ya kupokea mpira mrefu uliopigwa na kipa Aaron Kalambo kisha akaudonoa na kuzama nyavuni ukimuacha kipa Hussein Masalanga akihaha bila mafanikio.

Bao ambalo amefunga leo George Mpole ni la 15 kwenye ligi msimu huu ambapo amempita nyota wa Yanga, Fiston Mayele mwenye mabao 14 na kuongoza orodha ya wafumania nyavu kwenye ligi hiyo.

Ambapo ushindi huo wa mabao 2-0 unaifanya Geita Gold ifikishe pointi 39 na kukwea hadi nafasi ya tatu kutoka ya tano wakizipita Namungo na Azam FC zenye alama 37.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live