Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpole atabiriwa kumpiku Mayele mbio za Mfungaji Bora

Screenshot 20220504 120500 Mpole atabiriwa kumpiku Mayele mbio za Mfungaji Bora

Wed, 4 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Geita Gold FC, Fred Felix Minziro ameibuka na kusema kuwa Mshambuliaji wa klabu hiyo George Mpole ana nafasi kubwa ya kuwa Mfungaji Bora msimu huu mbele ya Fiston Mayele wa Young Africans.

Mpole kwa sasa anafukuzana na Fiston Mayele katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora, akiwa ameshafunga mabao 11, huku mpinzani wake akiwa na mabao 13.

Minziro anaamini Mpole ana nafasi kubwa ya kufunga zaidi katika michezo iliyosalia kwa msimu huu na kumpita Mayele na mwisho wa msimu kuwa mfungaji bora.

“Hakuna ugumu kwa Mpole kufikisha idadi kubwa ya mabao msimu huu kutokana na maarifa na jitihada anazozionyesha.”

“Muda wote akiwa uwanjani anafikiria kufunga kama alivyo Mayele na kimsingi ni ngumu kuwatofautisha washambuliaji hawa kwa muda huu kwani wanapokuwa uwanjani muda wowote unaweza kuona wakifunga na ndio maana namuona Mpole akifanya makubwa zaidi.” amesema Minziro

Huu ni msimu wa kwanza kwa George Mpole kucheza Ligi Kuu akiwa na klabu ya Geita Gold FC kama ilivyo kwa Mayele aliyesajiliwa Young Africans akitokea AS Vita ya kwao DR Congo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live