Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpole arejea kwenye makali yake

George Mpole Abadili Mpole arejea kwenye makali yake

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika mtanzania anayekipiga huko nchini Congo DR kunako Klabu ya St Eloi Lupopo amerejea katika makali yake baada ya kutoa assist 2 katika mechi iliyopita na kufunga magoli 2 kwenye mechi ya jana huko Congo DR dhidi ya wenyeji wao AS Dauphin kwenye mechi ya Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Mpole kabla ya kuibukia nchini Congo DR amewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na Geita Gold FC na kumshinda straika wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele, ambaye ametimkia Pyramids ya Misri.

Mpole baada ya kutua St Eloi Lupopo hakuwa akipata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza na wakati mwingine hakuwa akipata hata nafasi ya kukaa benchi hali ambayo imebadilika siku za hivi karibuni ambapo mchezaji huyo anaonekana kuwa tegemeo kikosini hapo.

Jana, Machi 24 amefunga magoli hayo dakika ya 43 na 85 na kuipa ushindi klabu yake. George Mpole kwenye michezo miwili ya mwisho akiwa na timu hiyo amehusika kwenye magoli 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live