Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpole apewa wiki moja Geita

George Mpole Training Mpole apewa wiki moja Geita

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Sakata linalomhusu mshambuliaji wa Geita Gold FC na mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, George Mpole linazidi kuchukua sura mpya baada ya staa huyo kutakiwa kuwasili katika kituo chake cha kazi ndani ya wiki moja.

Nyota huyo ameshindwa kuonekana kambini kwenye michezo mbalimbali ya timu hiyo kwa kile alichoeleza kuumwa huku baadhi ya taarifa zikidai mbali na madai hayo ila Mpole anadai stahiki zake za mshahara wa mwezi wa 10.

Baada ya sintofahamu taarifa za uhakika zinadai kuwa Mpole amepewa wiki moja za kuripoti kwenye kituo chake cha kazi ili kuendelea na programu za timu na kama atashindwa kuhudhuria atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

“Uongozi umemuita ili kujua changamoto inayomkabili kwa sababu amekuwa akisema anaumwa, lakini sisi hatujui hilo kwa kuwa yupo mbali na eneo la kufanyia kazi, hivyo tumemwandikia barua ya kujieleza,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliongeza kama atashindwa kufika kwa muda aliopewa basi uongozi utachukua hatua zaidi ikiwemo kumpeleka kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumshughulikia.

Akizungumza Kaimu Katibu Mkuu wa timu hiyo, Liberatus Pastory alisema wao kama viongozi lengo lao ni kuona nyota huyo anarejea kwenye kikosi chao ili kuwasaidia kwani wanatambua na kuthamini mchango wake.

Kwa upande wa Mpole alisema suala la kuitwa na viongozi wake wa juu analifahamu ila yeye atarudi tu pindi atakapopata ahueni ingawa kwa sasa yupo jijini Mwanza akiendelea na matibabu ambayo hakutaka kuyaweka wazi.

Mpole ndiye staa pekee ambaye hadi sasa hajawasili kambini kati ya wale walioripotiwa kutoweka kutokana na kudai stahiki zao huku wengine wakiwa ni Said Ntibazonkiza, Samson Sebusebu, Oscar Masai na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.

Chanzo: Mwanaspoti