Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpole, Kibu kuongoza mashambulizi Stars dhidi ya 'The Cranes'

Stars Vs Ug.jpeg Wachezaji wa Stars

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars, Kim Poulsen amemuazisha, George Mpole kuongoza mashambulizi katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.

Timu hizo zinatafuta nafasi hiyo ili kutinga kwenye fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.

Katika kikosi cha leo mbali na Mpole ila atashirikiana na mshambuliaji wenzake, Kibu Denis ikiwa ni mchezo muhimu kwa Stars inayopigania nafasi ya kuingia makundi kwa mara ya tatu.

Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kukutana na Uganda kwenye michuano ya kufuzu huku Stars ikishinda jumla ya mabao 3-1 na kuitoa 'The Cranes' katika fainali hizi zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini Ivory Coast 2009.

Hata hivyo Uganda ililipa kisasi hicho 2014 baada ya kuifunga Stars jumla ya mabao 4-1, katika fainali hizi zilizofanyika Afrika Kusini.

Kikosi kamili kinachoanza ni, Aishi Manula, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Kibwana Shomari, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Jonas Mkude, Salum Abubakar 'Sure Boy' Farid Mussa, Feisal Salum 'Fei Toto', George Mpole na Kibu Denis.

Wachezaji wa akiba ni, Aboutwalib Mshery, Pascal Msindo, Kennedy Juma, Mzamiru Yassin, Tepsie Evance, Anwar Jabir na Daniel Lyanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz