Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpo? Mo Salah ndiye bora duniani

 120347690 Hi069957080 Salah Mpo? Mo Salah ndiye bora duniani

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

LONDON, ENGLAND. CHAKO kipambe wanasema. Gwiji la Liverpool, Jamie Carragher anasema supastaa wa miamba hiyo ya Anfield, Mohamed Salah ndiye mchezaji bora duniani kwa sasa mbele ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Mo Salah ameanza msimu huu vizuri kabisa, akiwa moto kwenye kupachika mabao, ambapo hadi sasa ameshatikisa nyavu mara tizo katika mechi tisa alizocheza, ambapo juzi Jumapili alifunga bao matata kabisa dhidi ya Manchester City kwenye ligi.

Baada ya bao hilo la juhudi binafsi, Carragher alithubutu kusema Mo Salah ndiye mchezaji bora duniani kwa sasa.

Carragher alisema: “Sidhani kama kuna aliyebora Ulata kwa sasa zaidi yake, sioni kabisa. Nimemwona pia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, rekodi zake kwa wiki za karibuni, ni balaa kubwa.

“Huwezi kuhoji sana uwezo wake kutokana na kile anachokifanya Livetpool, lakini kwa sasa yupo kwenye kiwango bora sijawahi kuona.”

Carragher alisema kwa kiwango cha Salah anastahili kabisa kuwekwa kwenye orodha ya magwiji wa Anfield, akisema: “Kile ni kiwango cha dunia, ni mchezaji wa kiwango cha dunia. Nilisema hili wiki chache zilizopita, yeye ni mmoja wa wanasoka bora kabisa waliowahi kuichezea Liverpool.” Kwa ujumla wake, Salah amefunga mabao 134 katika mechi 212 alizochezea Liverpool, huku akiasisti mara 50.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz