Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpo? Kante anarudi Ulaya

Ng'olo Kante Man Award N’Golo Kante

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpo? N’Golo Kante amerudi.Na baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi mara mbili mfululizo zile za kwanza ilizocheza timu yake ya Ufaransa kwenye fainali za Euro 2024 huko Ujerumani, kazi ni kwa klabu za Ulaya sasa kuchangamkia huduma yake.

Kante, 33, amerejea kwenye kikosi cha Ufaransa baada ya miaka miwili na anachokionyesha ni kama vile hajawahi kuondoka.

Kiungo huyo mkabaji alikosa fainali za Kombe la Dunia 2022 kutokana na kuwa na maumivu ya misuli na baada ya hapo aliachana na Ligi Kuu England na kutimkia zake Saudi Arabia kujiunga na Al-Ittihad kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana.

Wakati wengi wakiamini Kante amekwenda Saudia kuvuna tu pesa, mambo ni tofauti kabisa, kiungo huyo anapiga soka la kibabe uwanjani.

“Nimefurahi kurudi kwenye buti zangu na kucheza kwenye ushindani mkubwa na ninavyopewa sapoti,” alisema Kante.

“Najisikia vizuri. Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwangu, hivyo nilikuwa na maandalizi mazuri kabla ya kuja hapa Ulaya, natumaini nitaendelea kuwa hivi. Kwa wachezaji wengine wanaotaka kurithi nafasi yangu wawepo tu, lakini mwenyewe nataka kuendelea na kujitolea kila kitu.”

Uwezo wake wa kucheza eneo kubwa la uwanja limemfanya atofautiane na wachezaji wengine na ndiyo maana mara zote amekuwa akishinda tuzo za mchezaji bora wa mechi kwenye mechi zote kubwa na zenye upinzani mkali.

Baada ya kung’ara kwenye Euro 2024, Kante aliulizwa kama anatoa nafasi ya kurudi tena kwenye soka la Ulaya na mwenyewe alisema hivi: “Sidhani kama maisha yangu ya kucheza Ulaya yamepita. Ningependa kurudi tena. Nilikuwa na mwaka mzuri sana Saudi Arabia. Kule kuna aina tofauti kabis aya soka na nimepata uzoefu tofauti, lakini nimefurahi kurudi Ufaransa. Nzuri sana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live