Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpo? Haaland ana ujumbe wenu huku

Haaland X Young Boys Erling Haaland

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Straika kiboko kabisa kwa kusukumia mipira nyavuni, Erling Haaland amechimba mkwara na kusema msimu huu atakuwa moto zaidi ya msimu uliopita.

Straika huyo wa Manchester City, Haaland alisema atakachokifanya ni kuwa bora zaidi ya msimu uliopita, wakati alipoisaidia timu yake kubeba mataji matatu, Ligi Kuu England, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Haaland alisema hayo baada ya kukosa Tuzo ya Ballon d’Or mbele ya Lionel Messi na kufanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya pili, akidai jambo hilo limemtia zaidi hasira ya kufanya kweli msimu huu.

Ukiweka kando kubeba mataji matatu, Haaland alifunga pia mabao 52 kwenye kikosi hicho cha Man City, huku akidai atakachofanya ni kuendelea pale alipoishia, tena kwa moto mkali zaidi. Kutokana na kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja, Haaland alinyakua tuzo ya Gerd Muller.

Alisema: “Ni heshima kubwa kupata tuzo hii ya Gerd Muller Trophy. Nisingeweza kufunga mabao yale msimu uliopita bila ya msaada wa wachezaji wenzangu, hivyo tuzo hii ni yetu sote. Napambana nifanye vizuri kwenye kila mechi na malengo ni kufanya vizuri zaidi msimu huu.”

Haaland tayari ameanza kwa kishindo kwenye Ligi Kuu England msimu huu, huku akifunga mabao 13 katika mechi 15 alizocheza kwenye michuano yote.

Chanzo: Mwanaspoti