Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpo? Erling Haaland katangaza vita EPL

Haaland Bao 2 Straika wa Manchester City, Erling Haaland

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Manchester City, Erling Haaland ametuma ujumbe wa vitisho kwa wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Haaland alisema tena kwa msisitizo kwamba Man City imejipanga kuwa bora zaidi msimu huu, huku yeye mwenyewe akihakikisha anakuwa straika bora. Man City imelenga kunasa taji la tano mfululizo la Ligi Kuu England, lakini inafahamu wazi itakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa timu za Arsenal, Liverpool na pengine Manchester United.

Lakini, Haaland - ambaye amefunga mabao 91 katika mechi 100 alizoitumikia Man City, ambayo msimu huu wa Ligi Kuu England imeanza kwa kuichapoa Chelsea mabao 2-0 kwenye mechi ya kwanza ya ligi, alisema kikosi kizima kimejiandaa kuwa bora zaidi mwaka huu.

Haaland, 24, alikiri kwamba yupo kwenye presha ya kufunga mabao mengi zaidi na kuleta mataji, huku akitakiwa kupandika kiwango chake.

Straika huyo wa Man City, Haaland alisema: “Haya ni maisha yangu kama mwanasoka – unakuwa na presha kila siku kutoka katika klabu, kwa mashabiki na kocha Pep Guardiola. Unapaswa kufanya ni kucheza kwa kiwango kizuri kuwafurahisha. Nataka kuboresha kiwango changu na kiwango cha timu. Nadhani tulicheza vizuri na tumeanza vyema. Tutakwenda mdogo mdogo mechi baada ya mechi.”

Haaland alisema kwenye kikosi chao kuna kundi kubwa la wachezaji wenye viwango bora kabisa kuhakikisha wanatetea taji lao.

Kocha wa Man City, Guardiola ameweka imani kubwa kwa mastaa kama Mbrazili mpya kikosini, Savinho na kinda Rico Lewis ambao walifanya vizuri sana kwenye mechi za pre-season wakati ambao Haaland alikuwa akivaa kitambaa cha unahodha.

Haaland alisema: “Tuna silaha changa matata kwelikweli na kuwa nahodha kwenye timu lilikuwa jambo la kuvutia sana, nilifurahia. Tuna nahodha mmoja kwenye timu, lakini kuna viongozi wengi sana kwenye kundi letu. Pengine huwezi kuliona hilo, lakini uhakika uliopo kwenye safu yetu ya mabeki inatupa hali ya kujiamini. Tuna watu, nafurahi kuwa hapa. Nipo tayari kwa vita.”

Chanzo: Mwanaspoti