Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpira uliotumika na Maradona kufunga goli la mkono wa Mungu kuuzwa kwa £2.5-3m

Mpira Wa Maradona Mpira uliotumika na Maradona kufunga goli la mkono wa Mungu kuuzwa kwa £2.5-3m

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: Bbc

Mpira uliotumiwa na Diego Maradona kufunga mabao mawili maarufu katika historia ya soka utapigwa mnada

Mpira wa mechi hiyo ya robo fainali ya Kombe la Dunia la 1986 kati ya Uingereza na Argentina unakadiriwa kuwa na bei ya £2.5m hadi £3m.

Unauzwa na Ali Bin Nasser, mwamuzi wa Tunisia aliyeruhusu bao la Maradona la 'Mkono wa Mungu' wakati wa mechi hiyo.

Bin Nasser alisema: "Mpira huu ni sehemu ya historia ya soka - ni wakati mwafaka kuusambaza kwa ulimwengu."

Mpira huo ulitumika kwa dakika 90 za mechi, ambayo inasalia kuwa moja ya mashindano ya wazi na yenye utata katika historia ya Kombe la Dunia.

Maradona alifunga bao la kwanza kwa kuupiga mpira kwa kutumia mkono juu ya kipa wa Uingereza Peter Shilton.

Bin Nasser hakuona kwamba Maradona alifunga bao lile kwa kiutumia mkono na hivyo akaliruhusu bao hilo kusimama, ambapo mchezaji huyo alilitaja bao hilo kuwa lilifungwa kwa mkono wa Mungu".

Goli la pili la Maradona kwenye mechi hiyo limejulikana kama 'bao la karne', ambapo aliwapiga chenga wachezaji watano wa England Pamoja na kipa wake na baadaye akafunga.

Chanzo: Bbc