Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpira ni mkakati, ahadi ya pesa haitoshi - Dewji

Simba Vs Ahly 1 0.jpeg Mpira ni mkakati, ahadi ya pesa haitoshi - Dewji

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa mfadhili wa Simba, Azim Dewji amegusia namna ambavyo klabu hiyo imetoa motisha kwa wachezaji wake kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Amesema tayari wachezaji warnajua kuwa, kila mmoja atapata Tsh. 100 milioni iwapo watafanikiwa kufika hatua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini tayari zipo Tsh. 650 milioni iwapo watafanikiwa kuitoa Al Ahly na kufuzu Nusu Fainali.

Pamoja na hayo yote, Azim Dewji amesisitiza kuwa, ahadi ya pesa pekee haiwezi kuwa chachu ya mafanikio bali mikakati sahihi ndio inaweza kuisaidia timu kufikia malengo waliyojiwekea.

"Sio pesa kepee ndio itaifanya Simba ishinde, kama wapenzi walikuwa hawajui nataka wajue. Wachezaji waliahidiwa fedha kabla ya mechi ya kwanza kwamba wakivuka Robo Fainali watapafa milioni 650."

"Kwa hiyo bado ile milioni 650 ipo palepale kwa sababu waliambiwa wakivuka, licha ya kupoteza mchezo wa kwanza kama watashinda mchezo wa pili na kuwatoa Al Ahly watachukua hizo fedha."

"Mipango ilivyo, kama Simba itafika Fainali huenda kila mchezaji akapafa milioni 100. Maana kama wameahidiwa milioni 650 wakifika Nusu Fainali, kufika Fainali wataahidiwa si chini ya bilioni moja."

"Na wakifika Fainali hawawezi kuahidiwa bilioni moja ili wachukue ubingwa, wataahidiwa bilioni moja na nusu, sasa ukifanya majumuisho ya fedha watakazopata kuanzia Nusu Fainali hadi Fainali unakuta ni zaidi ya bilioni tatu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live