Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpinzani wa Mayele; Mwamba huyu hapa!

Xb Mayele Lakay Mpinzani wa Mayele; Mwamba huyu hapa!

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fagrie Lakay (26) ni raia wa Afrika Kusini ambaye anakipiga katika Klabu ya ya Pyramids ya nchini Misri ndiye mpinzani mkuu wa namba na Fiston Mayele katika kikosi hicho.

Lakay ndiye kinara wa magoli wa klabu ya Pyramid huku akishika nafasi ya nne kwa wafungaji Bora wa Ligi kuu nchini Misri msimu uliopita, akiwa amefanikiwa kutia nyavuni magoli 10 katika michezo 30 aliyoicheza.

Fiston Mayele raia wa Congo Dr msimu jana alikuwa Top Score wa Ligi Kuu nchini Tanzania akifunga Magoli kuminasaba {17} akiwa na Klabu ya Young Africans huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya CAFCC akiwa na mabao 7.

Lakay amewahi kuzitumikia klabu za Cape Town City, Bidvest Wits FC, SuperSport Utd, Ajax Cape Town, Santos FC kwa nyakati tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live