Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpanzu haendi Simba, dili limekufa, bosi athibitisha

Mo Dewji X Mpanzu Mpanzu haendi Simba, dili limekufa, bosi athibitisha

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dili la uhamisho wa kiungo mshambuliaji wa AS Viya ya Congo DR, Elie Mpanzu kwenda Klabu ya Simba, umeshindikana kabisa, hii imethibitishwa jana usiku na mabosi wa Simba SC.

Mpanzu alikuwa akihusishwa kujiunga na Simba kama mbadala wa Kibu Denis ambaye ametimka klabuni hapo na kwenda Ulaya kujaribu bahati yake huko na kuiacha timu yake kwenye njia panda licha ya kusaini mkataba wa miaka miwili hivi karibuni.

"Mpanzu haji tena. Tulijaribu kila tuwezalo lakini labda haikutosha. Inasumbua sana. Lakini tuone, natumai tutasajili mchezaji mwingine badala yake lakini pengine, hatakuwa kwenye kiwango na ubora sawa na Mpanzu," amesema moja ya viongozi wa Simba.

Mpanzu alishatoa mwelekezo wake kwa Simba na alikuwa tayari kuhama lakini mgogoro ndani ya klabu Klabu ya AS Vita pamoja Simba kuwasilisha ofa yao wakiwa wamechelewa (ambayo lilikataliwa) ndiko kumezuia dili hilo na kumlazimu Mpanzu kutafuta kwingine ambapo anaelezwa kuwa ametimkia KRC Genk ya Ubelgiji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live