Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpanzu afunguka kila kitu dili lake kutua Simba

Mo Dewji X Mpanzu Elie Mpanzu na Mo Dewji

Sun, 28 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache tangu ifahamike kwamba mabosi wa Simba wamerejesha majeshi upya kwa winga Mkongomani, Ellie Mpanzu ili kumsajili kikosini kuziba nafasi ya Kibu Denis, nyota huyo wa AS Vita amemaliza utata kwa kuzungumza na Mwanasopoti na kuanika dili lote lilivyo na kutoa msimamo wake.

Mwanaspoti liliwajulisha mapema kwamba dili la Mpanzu Simba ni kama limekwama kutokana na ishu ya maokoto, kabla ya mabosi w Simba kumrudia kutokana na kuibuka biashara ya Kibu kuwa katika hatua nzuri ya kutua Kristiansund BK ya Norway na ilikuwa na hesabu za kuachana ama na Freddy Michael au Willy Onana inayeelezwa kuna timu Qatar inamtaka kwa sasa.

Simba ilikuwa ikimpigia hesabu nyota huyo, kiasi cha kurudi kwa mara ya tatu sasa AS Vita ya DR Congo, lakini dau lililowekwa na klabu hiyo ya kutaka Dola 250,000 (zaidi ya Sh 500 milioni) kumuachia liliwazuia Msimbazi kumbeba mapema kama ilivyofanya kwa nyota wengine waliopo kambini Misri.

Simba ilikuwa ikimuona Mpanzu kama mbadala sahihi wa Kibu kama atapata timu nje kutokana na aina yao ya kiuchezaji, wakiwa na kasi, nguvu na kutochoka haraka uwanjani mbali na kusaidia kukaba.

Hata hivyo, Mwanaspoti iliamua kumsaka Mpanzu mwenye mkataba wa mwaka mmoja na AS Vita na mwenyewe kufunguka ukweli wa kufuatwa na Simba na kuweka bayana na kutoa msimamo alionao, akiitaja klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji aliyowahi kuitumikia Mbwana Samatta

Akizungumza na Mwanaspoti, Mpanzu (22) alisema ni kweli Simba imekuwa ikimtaka na ilikuwa ikifanya mazungumzo na mabosi wa AS Vita, lakini msimamo wake ni kwenda kucheza soka Ulaya na sio Msimbazi.

Mpanzu alifichua sababu hasa ya msimamo huo wa kuikacha Simba na kutaka kwenda Ubelgiji kukipiga Genk ni familia yake sambamba na ndoto za muda mrefu alizonazo za kucheza Ulaya.

“Familia ilinishauri kuishi katika ndoto zangu na sio kuangalia maslahi kila wakati, hiyo tu imekuwa sababu yenye nguvu sana moyoni mwangu, kwani nataka kufanya kazi kwa furaha,” alisema Mpanzu na kuongeza;

“Nilitaka kuja Simba kwani nayo ni timu kubwa na nzuri, lakini kuna wakati nilitakiwa kufikiria mbele zaidi kwani hata kama ningekuja huko bado ningekuwa naiwaza ndoto yangu ya kuchezea Ulaya.”

Simba ilikuwa tayari imeshakubaliana na Mpanzu kusaini mkataba wa miaka miwili, lakini baadaye vigogo wanaommiliki winga huyo akiwemo moja ya matajiri wa AS Vita, aliingilia kati dili hilo na kumzuia staa huyo kusaini kwa kutaka dau nono zaidi na ndilo lililowarudisha nyuma vigogo wa Msimbazi.

Kutokuja kwa Mpanzu ndani ya Simba kumewapa shavu Willy Onana na Freddy Koublan kusalia Msimbazi, kwani awali mmoja ilikuwa lazima ampishe Mkongomani huyo, huku ikielezwa Onana alikuwa na nafasi kubwa kwa vile kuna ofa kutoka Qatar.

Kwa sasa Simba ina wachezaji 12 kwa mujibu wa kanuni ya nyota wa kigeni, baada ya kusaliwa na wachezaji watano waliokuwapo msimu uliopita akiwamo kipa Ayoub Lakred, Che Fondoh Malone, Fabrice Ngoma, Freddy na Onana walioungana na wapya saba.

Nyota hao saba wapya ni Joshua Mutale, Steven Mukwala, Augustine Okejepha, Valentin Nouma, Debora Mavambo, Jean Charles Ahoua na Chamou Karaboue.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live