Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpaka aende kwa Mapacha wa Kariakoo ndio mtamuelewa?

Sospeter Bajana Haimbwi Kiungo wa Azam FC, Sospeter Bajana

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna mahala watanzania macho yetu tumeyaelekeza sana Kariakoo pekee hatutaki kuangaza na Mbagala japo kidogo tukaone namna Baraka na ma ajabu ya mwenyezi kwenye miguu ya Sospeter Bajana.

Bajana hasemwi sana kama akina Pacome sjui akina Kibu Dee kwasababu watu wa kumsemea Bajana ni vile wachache Ibwe na Zakazakazi Pakeee baada ya hapo hamna mwengine.

Ila nakuhakiishia ukikaa na Kiungo wa Manchester United Sofyane Amrabat ukamuuliza kuhusu Tanzania neno lake la mwanzo anaweza kutaja Bajana.

Bajana apewe japo siku moja tu acheze kwenye timu ya Kariakoo yenye timu Bora kabisa hiyo siku ndio tutashuhudia Viapo vingi vya mashabiki vikisema hakuna Holding Midfielder Kama Bajana.

Kama Amrabat amekubali na yupo Manchester wewe nani ukatae Shekh.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live