Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moyes aweka ngumu uhamisho wa Declan Rice West Ham

Moyes Dfgg.jpeg Kocha wa West Ham

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Westham United David Moyes amesema kua kiungo mahiri ndani ya klabu hiyo Declan Rice atabakia ndani ya klabu hiyo kama hakuna timu ambayo itafika bei ya mchezaji huyo.

Kocha Moyes anasema anaamini kiungo huyo yupo sehemu sahihi sana kwa wakati huu na kama mchezaji huyo ataondoka klabuni hapo basi itahitajika klabu inayomuhitaji wanapaswa kufika kiwango cha bei ambacho kimewekwa na klabu hiyo ya wagonga nyundo wa London

Declan Rice amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya West Ham kwa takribani miaka mitatu sasa na amekua akivivutia vilabu vingi barani ulaya haswa ndani ya Uingereza, Lakini kwa misimu kadhaa nyuma alikua anahusishwa zaidi na klabu ya Manchester United.

Kiungo huyo amekua na misimu bora sana chini ya kocha David Moyes na anavutiwa sana na kiungo huyo vilevile ameweka wazi anatamani kumuona mchezaji huyo akiendelea kuitumikia klabu ya West Ham United kwa misimu kadhaa mbele lakini kuna kipengele kinachomruhusu mchezaji kuondoka klabuni hapo kama ofa nzuri itawafikia.

Klabu ya Arsenal kwasasa inaelezwa ndio inaongoza mbio za kunasa mbio za kumuwania kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza ili kukiboresha kikosi chao zaidi kwenye eneo la katikati, Kwani imeonekana mara kadhaa akikosekana kiungo Thomas Partey klabu hiyo inapata wakati mgumu kwenye eneo la katikati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live