Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mourinho kathibitisha staa ambaye hatokuwa nae kwa miezi mitatu

242 Jose Mourinho Man Utd 2017 Qpcc7rzvk4tx1gfo5aqflr3pz 660x400 TZW

Fri, 15 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Kocha wa club ya Manchester United Jose Mourinho leo Ijumaa ya December 15 2017 amemtaja staa wa soka wa kimataifa wa Ivory Coast Eric Bailly kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu.

Jose Mourinho amethibitisha beki wake Eric Bailly atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu kufuatia jeraha la enka alilolipata wakati wa game ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea na Man United walipoteza kwa goli 1-0.

Eric Bailly ameripotiwa kuhitajika kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na kuhitaji upasuaji wa jeraha hilo “Anahitaji kufanyiwa upasuaji ndio uamuzi uliyofanywa na sijasema kwamba atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia ila atakuwa nje kwa miezi miwili hadi mitatu”>>> Mourinho

UTANI: Haji Manara kwa wapinzani wao Yanga baada ya Simba kumpata MO Dewji

Chanzo: millardayo.com