Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mourinho kaanza kuliamsha Uturuki

Jose Mournhooo Mourinho kaanza kuliamsha Uturuki

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Jose Mourinho ni yuleyule, habadiliki baada ya kuwasha moto kwenye mechi yake ya kwanza tu Turkish Super Lig na kuamsha vurugu.

Kocha huyo aliyejipachika jina la The Special One kwa sasa ni bosi wa Fenerbahce na haikumchukua muda mrefu kuliamsha kwenye ligi hiyo wakati wa mchezo wa kwanza wa ligi ya ndani ya timu yake msimu huu.

Zikiwa zimepita dakika 20 baada ya mechi kuanza, Mourinho aliliamsha kwa kulumbana na mwamuzi.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Manchester United, Real Madrid, Inter Milan, FC Porto na Tottenham alikasirishwa baada ya uamuzi kwenda kinyume na timu yake, ambapo alianza kupiga kelele na kumfokea mwamuzi wa akiba.

Jambo hilo lilimfanya Mourinho aonyeshwe kadi ya njano na mwamuzi wa mchezo Atilla Karaoglan.

Na mashabiki walipendezwa na jambo hilo, ambapo moja alisema: “Jose, tafadhali, usibadilike.”

Mwingine aliongeza: “Utakwenda kuwa msimu mrefu sana.”

Na shabiki wa tatu alisema: “Mourinho atakwenda kuwa sinema nzuri sana msimu wote, lazima nitazame.”

Licha ya jambo hilo la Mourinho, Fenerbahce ilishinda 1-0 mechi hiyo dhidi ya Adana Demirspor, shukrani kwa bao la staa wa zamani wa Ligi Kuu England, Edin Dzeko. Ilikuwa mechi ya kwanza ya msimu mpya wa Turkish Super Lig na tayari mambo yanaonekana kwenda sawa kwa Fenerbahce.

Chanzo: Mwanaspoti