Kocha mreno, Jose Mourinho ameipongeza timu yake ya Roma licha ya kushindwa kwao Serie A na Napoli siku ya Jumapili.
wachezaji wake walionekana kutofurahishwa na kulazimika kupiga picha ya timu ambayo bosi huyo wa zamani wa Chelsea aliipakia kwenye Instagram.
Roma walichuana na vinara wa ligi hiyo Napoli na kupoteza kwa mabao 2-1 kwa bao la dakika ya 86 lililofungwa na Giovanni Simeone.
Kipigo hicho kilikuwa cha kuhuzunisha kwa Roma, ambao wanapigania kurejea katika nafasi nne za juu na kurejea Ligi ya Mabingwa, wakiwa wamepiga hatua kubwa chini ya Mourinho tangu 2021.
Licha ya kushindwa, kulikuwa na chapisho kutoka Instagram ya Mourinho ambapo alikuwa akiisifu timu yake, jambo ambalo ni nadra baada ya kushindwa
Aliweka picha ya timu yake ikiwa na maandishi: “Ni TIMU gani ROHO gani UTENDAJI. Twende… Tuonane Jumatano kwenye Olimpico.”
Picha hiyo ilionyesha nyota wengi wa Roma akiwemo Tammy Abraham, Paulo Dybala, Andrea Belotti na Stephen El Sharaawy – wakiwa wamekata tamaa pamoja na wakufunzi wao wengine.
Katika vyombo vya habari, Mourinho pia alifurahishwa na uchezaji wa timu yake: “Tulicheza soka zuri sana tangu dakika ya kwanza. Kulikuwa na kipindi cha dakika 10-15 baada ya bao la Osimhen tulipohisi dhuluma ya kwenda chini 1-0.
“Mbali na hayo, timu ilikuwa ikidhibiti kila wakati, ikikabia juu, iliokoa mpira, ililinda vyema,” alisema kwa DAZN baada ya mchezo.
Hivi karibuni kumekuwa na ripoti kwamba Mourinho hana furaha akiwa Roma na anatafuta kurejea Uingereza msimu ujao.