Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mourinho awapiga kijembe Spurs, Conte

767474 Jose Mourinho Troubled Reuters?fit=1280%2C720&ssl=1 Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho, amehoji uamuzi wa klabu yake ya zamani ya Tottenham Hotspur kumbadilisha Nuno Espirito Santo na Antonio Conte.

Conte raia wa Italia alisaini mkataba wa miezi 18 kuinoa Spurs Jumanne baada ya Nuno kutupiwa virago akiwa ameanza msimu huu kwa kushinda mechi tano na kupoteza tano kati ya 10 za Ligi Kuu England.

Kocha huyo wa zamani wa Wolves kipindi chake cha miezi minne ya kukaa na klabu hiyo ya London Kaskazini kilifikia mwisho Jumatatu baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa timu ya zamani ya Mourinho, Manchester United.

Wakati alipoulizwa kama Spurs kumchukua Conte kunaweza kuifanya Tottenham kuwa imara, Mourinho aliiambia Sky Sport: “Yeye ni kocha mzuri, lakini Nuno Espirito Santo pia ni kocha mzuri sana ambaye amefanya makubwa kwa miaka minne au mitano pale Wolverhampton.

“Siwezi kusema kwamba, Tottenham wana kocha mzuri hivi sasa, wamefanya hivyo kabla. Wanaye sasa na walifanya hivyo.”

Kama ilivyo kwa Mourinho, Conte alifurahia mafanikio muda uliopita kwenye soka la Uingereza akiwa na Chelsea, ambapo aliwaongoza kutwaa taji la Ligi Kuu na FA kwa kipindi cha misimu miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live