Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mourinho atoa sharti moja tu kutua Fenerbahce

Jose Mourinho Amefikia Makubaliano Na Fenerbahce Kandarasi Ya Miaka 2.jpeg Jose Mourinho

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Jose Mourinho amejiandaa kwenda kuchukua mikoba ya kuinoa Fenerbahce kwa sharti moja tu.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 61, amekuwa hana kazi tangu alipoachana na AS Roma, Januari mwaka huu. Na sasa amekubali kurejea kwenye mikoba ya kuinoa miamba hiyo ya Uturuki.

Mourinho alifikia makubaliano ya kwenda kuinoa Fenerbahce wiki hii iliyomalizika. Mkataba wa miaka miwili na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi umefikiwa makubaliano na pande zote.

Hata hivyo, Calcio Mercato linaripoti kwamba ‘Special One’ anataka kwenye mkataba huo kuwekwe kipengele maalumu kinachomruhusu muda wowote kuondoka endapo itatokea ofa ya kwenda kuinoa timu ya taifa ya Ureno.

Kocha huyo wa zamani wa Manchester United, Chelsea na Tottenham aliwahi kuzipuuzia ofa mbili za kwenda kuinoa timu hiyo ya taifa yenye mastaa kibao makini.

Mourinho alimwambia Fabrizio Romano: “Nilifunguliwa mlango wa kwenda kuinoa Ureno mara mbili. Mara ya kwanza nilipokuwa Real Madrid, lakini Florentino Perez alikataa. Mara ya pili, nilipokuwa Roma, niligoma na hiyo sijutii kwa sababu nilikuwa na sababu zenye maana.”

Mourinho aliwahi kuzinoa klabu tatu za Ureno - Porto, Benfica na U.D. Leiria, lakini bado hajawahi kuinoa timu ya taifa la nchi yake na hicho ndicho kitu anachotaka.

Chanzo: Mwanaspoti