Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mourinho amtaja Ten Hag ishu ya Sancho

Sancho Aed Mourinho amtaja Ten Hag ishu ya Sancho

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jose Mourinho amemshutumu Erik ten Hag kwamba ndiye tatizo, hajui namna bora ya kumfanya winga Jadon Sancho acheze kwa kiwango cha juu Manchester United.

Sancho, 24, ameonekana ni mchezaji tofauti kabisa baada ya kwenda kujiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo kwenye dirisha la Januari, alipocheza kwa kiwango bora chini ya kocha Edin Terzic, alipoisaidia kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuchapwa na Real Madrid 2-0 uwanjani Wembley, Jumamosi iliyopita.

Lakini, winga huyo hakuwa na wakati mzuri Old Trafford, ambako alitibuana na Ten Hag, baada ya kudai kwamba hakuwa vizuri mazoezini Septemba na kukosa mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal kwenye duru la kwanza.

Sancho alimpinga kocha wake na kusema hadharani ni muongo na anachojaribu ni kumfanya kuwa mbuzi wa kafara, kitu kilichomsababisha awekwe kando kwenye mazoezi ya timu hiyo hasa baada ya winga huyo kugoma kumwomba kocha msamaha.

Ishu hiyo imewagawanya watu, ambapo kocha Mourinho alisema Ten Hag ndiye wa kulaumiwa kwa kuwa hajui namna nzuri ya kumfanya Sancho ang’are uwanjani.

Mourinho alisema kuhusu Sancho: “Kama mchezaji tunafahamu kipaji chake. Ni kweli kijana amefanya makosa. Lakini, ukweli kocha wake ameshindwa kupata namna bora ya kumtumia. Nadhani kwa kesi hii, United itajaribu kufanya tathmini ya kile kilichotokea.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live