Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mourinho ampiga kijembe Pep Guardiola

Mourinho X Phillips.jpeg Mourinho ampiga kijembe Pep Guardiola

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho amemtupia kijembe Pep Guardiola wa Man City kuhusu uwezo wake wa kutumia pesa nyingi kununua wachezaji wapya huku akisikitikia klabu yake AS Roma kukosa pesa za kusajili wachezaji.

Itakumbukwa siku za hivi karibuni Meneja wa Man City, Pep Guardiola alipokiri waziwazi kwamba kiungo wake Kalvin Phillips anaweza kuondoka klabuni mwezi Januari.

“Sio kwamba naona wivu, lakini Man City walilipa euro milioni 80 kwa ajili ya Kalvin Phillips na sasa Pep amesema ni bora aondoke Januari. Kwa hiyo ataondoka na watapata mchezaji mwingine.” Amesema Mourinho.

“Kwa upande wetu ni tofauti sana. Tungependa mchezaji mmoja, wawili, watatu au wanne... hata hivyo, si rahisi kwetu kufanya hivyo. Tukileta beki Januari, tayari nitakuwa na furaha. “

“Lakini ukiniuliza ikiwa ningependa zaidi ya hayo, bila shaka ningependa zaidi, lakini haiwezekani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live