Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mourinho agoma Zaniolo kuondoka Roma

Zaniolo Mourinho Roma Mourinho agoma Zaniolo kuondoka Roma

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jose Mourinho anaamini kuwa Roma wanaweza kumzuia Nicolo Zaniolo huku kiungo huyo wa kati wa Italia akishinikiza kuhama kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na vilabu mbalimbali lakini hasa Tottenham, timu ya zamani ya Mourinho, na kocha mkuu wa Roma anafahamu vyema kwamba kichwa cha Zaniolo hakijatulia kwa sasa..

Zaniolo hakuchezeshwa katika ushindi wa 2-0 wa Roma dhidi ya Spezia kwenye Serie A juzi , huku mkurugenzi wa klabu Tiago Pinto akisema kabla ya mchezo huo mchezaji huyo ameweka maslahi yake binafsi mbele ya timu kwa kuamua kutoshiriki.

Mourinho alisema:

“Mkurugenzi alizungumza kabla ya mechi, na alifanya hivyo vizuri. Jambo muhimu leo ​​ni kushinda na utendaji mzuri wa timu. Nina maoni yangu nadhani atakaa hapa Februari, lakini soko lipo wazi anataka kuondoka.”

Kuonyesha hamu haimaanishi kuondoka. Kawaida mchezaji anapotaka kuondoka ina maana kwamba kuna ofa muhimu nyuma yake, lakini sivyo. Hakuna kitu kwenye meza, hakuna kitu ambacho klabu inaweza kukubali. Alisema Mourinho.

Akiongea na mtangazaji wa DAZN, Mourinho aliongeza kuwa ana uhusiano mzuri sana naye, kwani amekuwa akijaribu kumsaidia. Amefanya juhudi kubwa na kwasababu hiyo amekuwa akimtetea kila mara hata anapokosolewa kwa sababu ya mabao machache na pasi za mbaao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live