Sat, 25 Dec 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Ripoti kutoka nchini Nigeria zinadai kuwa Boss wa zamani wa Chelsea, Manchester United na Tottenham Jose Mourinho amefanya mazungumzo na Nigeria kuhusu nafasi ya Umeneja wa timu yao ya Taifa.
Timu hiyo inatafuta Meneja mpya baada ya kumfuta kazi Gernot Rohr muda mfupi baada ya matokeo yao yasiyoridhisha huko Cape Verde.
Kwa sasa klabu hiyo inaongozwa na kocha wa muda Augustine Eguavoen.
Rais wa Shirikisho la soka nchini Nigeria Amaju Pinnick amedai kuwa wanatarajia kumtangaza Meneja mpya kabla ya michuano ya AFCON kuanza na ameashiria kuwa wamekuwa na mazungumzo na Mourinho.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live