Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mount hakupata majeraha, ni mipango ya

Mason Mount Inj.jfif Mason Mount

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Klabu ya Manchester United, Mason Mount siku ya jana alirejea uwanjani katika mchezo wao dhidi ya Crystal Palace Football Club baada ya kukaa nje kwa takribani mwezi mmoja kwa majeraha.

Lakini furaha ya mashabiki ilikatika baada ya kutolewa wakati wa mapumziko huku nafasi yake ikichukuliwa na Victor Lindeloef.

Hata hivyo mashabiki wa klabu hiyo walidhani huenda amepata jeraha tena lakini timu hiyo imethibitisha kuwa hana jeraha lolote na kubainisha kwamba mabadiliko hayo yalipangwa tangu mwanzo na kocha wa timu hiyo Ten Hag kwa ajili ya kumrejesha taratibu kwenye kikosi baada ya majeraha yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live