Sat, 14 Jan 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mshambuliaji wa Borusia Dortmund ya Ujerumani, Youssoufa Moukoko amekutwa na kashfa ya kughushi umri wake huku ikidaiwa kuwa umri wake halisi ni miaka 22 badala ya 18 ambao amekuwa akidhaniwa.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizotolewa na baba wa kambo wa nyota huyo jina lake halisi ni Youssoufa Mohamadou akiwa Cameroon na alizaliwa mwaka 2000 kabla ya kuasiliwa na kuishi na wazazi walezi huko Ujerumani.
Ikumbukwe Cameroon imeingia kwenye kashfa ya udanganyifu wa umri baada ya wachezaji 21 kati ya 32 wa umri chini ya miaka 17 waliopitia vipimo vya umri kufeli vipimo hivyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live