Rais wa Shirikisho la Kandanda Africa (Caf), Patrice Motsepe, ameimwagia sifa Ivory Coast, akisema nchi hiyo mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika ni ya “kipekee”.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Abidjan kabla ya mchezo wa fainali siku ya Jumapili kati ya Ivory Coast dhidi ya Nigeria, Motsepe amesema karibu watu bilioni mbili duniani wametazama michuano hiyo.
Mkuu wa idara ya mawasiliano wa Caf, Lux September amesema michuano hii inaelekea kuwa moja ya michuano “iliyofanikiwa zaidi kibiashara”.
Akizungumzia ishara walizozifanya wachezaji wa DRC uwanjani kabla ya kupoteza mchezo wao wa nusu fainali, Bwana Motsepe amesema “watu wa DRC wapo mioyoni mwetu na kuwa Caf ina “jukumu” kwa watu walioathirika na mizozo, mzozo ambao amekiri kuwa unaathiri pia nchi nyingine ikiwemo Rwanda.
Aidha, bwana Motsepe ameahidi kutembelea maeneo hayo.