Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto mpya Yanga ni noma

Yanga Pic Data Moto mpya Yanga ni noma

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Olipa AssaMore by this AuthorBy Oliver AlbertMore by this Author MWALIMU Alex Kashasha ameangalia moto wa Yanga kwenye Ligi Kuu Bara, halafu akamuangalia na Saido Ntibazonkiza kisha akacheka na kusisitiza kwamba watasumbua sana katika mzunguko wa pili.

Kashasha ambaye kitaaluma ni kocha amesisitiza kwamba Saido akizoea kidogo tu halafu Kocha Cedrick Kaze akapata straika mwingine pale mbele, patanoga zaidi.

Siyo Kashasha tu, straika matata wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel amevutiwa na mzuka wa mastaa wa Yanga na kukiri kwamba msimu huu utakuwa moto sana hasa kwenye mzunguko wa pili ulioanza sasa.

Gabriel anaamini kwamba Simba ikitoka kimataifa itakuja na kasi pia ambayo itaongeza utamu kwenye ligi hiyo ambayo Azam FC na Namungo FC pia wameipania.

Mwalimu Kashasha alisema kocha wa Yanga, Kaze anajitafsiri miguuni mwa wachezaji, kujitambulisha mbinu na uwezo wake katika kufundisha.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz