Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto kuwaka England, wababe wakikamatana viwanjani leo

Trsttdgc Moto kuwaka England, wababe wakikamatana viwanjani leo

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Leo ni leo. Hicho ndicho kinachoihusu Manchester United wakati itakaposhuka uwanjani Craven Cottage kukipiga dhidi ya Fulham kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Man United inahitaji kushinda mchezo huo ili kupunguza presha kidogo kwa kocha wake, Erik ten Hag - baada ya timu kuwa kwenye kiwango cha hovyo sana msimu huu, ambapo kwenye mechi 10 ilizocheza msimu huu, imepoteza tano.

Leo hii itacheza mchana ugenini kwa Fulham, huku rekodi zikiibeba Man United ambapo katika mechi 32 ilizowahi kukutana kwenye Ligi Kuu England, wababe hao wa Old Trafford wameshinda 23, mara 13 wakiwa nyumbani na 10 ugenini, huku Fulham imeshinda tatu tu, mbili nyumbani na moja ugenini.

Mechi tano za mwisho kukutana, Man United imeshinda nne na sare moja.

Hata hivyo, viwango vyao vya msimu huu ndivyo vinavyoibua mjadala. Itakuwaje? Man United itajinasua kwenye kuwa kichekesho? Ngoja tuone.

Manchester City itakuwa na fursa ya kurejea kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England endapo kama itafanikiwa kushinda dhidi ya Bournemouth katika mchezo utakaofanyika Etihad. Vijana hao wa Pep Guardiola wanashika nafasi ya tatu, pointi mbili nyuma ya vinara Tottenham Hotspur, ambayo haitacheza hadi keshokutwa Jumatatu itakapokipiga dhidi ya Chelsea.

Rekodi zinaonyesha kwamba Man City na Bournemouth zimekutana mara 12 kwenye Ligi Kuu England, huku wababe hao wa Etihad wakishinda mechi zote hizo, sita nyumbani na sita nyingine ugenini. Ushindi wa leo utawafanya kufikisha kufikisha pointi 27 na kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi na baada ya hapo itasikilizia matokeo ya Arsenal na Newcastle United huko St James’ Park.

Arsenal imeizidi Man City kwa mabao ya kufunga, lakini jeshi hilo la Kocha Mikel Arteta litakuwa na kibarua kigumu baadaye leo kwa kumenyana na Newcastle United, ambayo imekuwa ya moto.

Rekodi zinaonyesha kwamba Arsenal na Newcastle United zimekutana mara 56 kwenye Ligi Kuu England, sare 11, huku The Gunners ikishinda 34, mara 21 nyumbani na 13 ugenini, wakati Newcastle imeshinda 11, saba nyumbani na nne ugenini. Mechi tatu za mwisho walizokutana, Newcastle imeshinda moja, Arsenal moja na sare moja.

Kuhusu Spurs na Chelsea vita yao itakuwa balaa, London derby. Spurs imekuwa kwenye ubora mkubwa, ikiongoza ligi, lakini itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kazi ya kusaka ushindi tu kama inataka kurudi kileleni endapo kama Man City na Arsenal zitakuwa zimeshinda mechi zake.

Rekodi zinavyosoma, Spurs na The Blues zimekutana mara 62 kwenye Ligi Kuu England, huku Chelsea ikishinda 33, mara 19 nyumbani na 14 ugenini, huku Spurs ikishinda nane tu, saba nyumbani na moja ugenini. Mechi 21 sare.

Mechi nyingine zitakazopigwa leo, Brentford itakuwa nyumbani kucheza na West Ham United, wakati Burnley itakuwa na shughuli pevu mbele ya Crystal Palace huku Everton ikimaliza ubishi na wabishi Brighton. Sheffield United yenye msala mkubwa msimu huu, itakuwa nyumbani kucheza na Wolves.

Kesho, Jumapili kutakuwa na mechi mbili tu, ambapo Nottingham Forest itakuwa City Ground kukipiga na Aston Villa ya Unai Emery, huku Luton Town ikiwa na kasheshe la kuikaribisha Liverpool inayosaka ubingwa wa Ligi Kuu England kimyakimya msimu huu.

Hii ni mechi ya kwanza kwa Luton na Liverpool kukutana kwenye Ligi Kuu England, huku vijana hao wa Kocha Jurgen Klopp wakisaka pointi za kuiondoa Spurs kwenye ile nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu England. Mambo ni moto.

Chanzo: Mwanaspoti