Kocha wa zamani wa Mamelodi Sondowns, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini amesaini kusaini mkataba wa muda mfupi wa miezi minne na klabu ya Abha inayoshiriki Ligi ya Kuu ya Saudi Arabia.
Mosimane ambaye kabla ya kusaini dili hilo alikuwa anakinoa kikosi cha Al Wahda ya Falme za Kiarabu (UAE) aliwahi kukinoa pia kikosi cha cha Al Ahli ya Saudi Arabia kabla ya kuondoka kutokana na kutolipwa mshahara.
Akiwa na Al Ahli, aliipandisha kucheza Ligi Kuu Saudi Arabia.
Awali Abha ilitaka kumpa Kocha huyo mkataba wa miezi 18, lakini uongozi wake ulichagua mkataba wa muda mfupi.
Kwa mujibu wa Sunday World, taarifa hiyo imetolewa na Afisa Masoko na Michezo wa MT, "Ninathibitishia Kocha Pitso amesaini rasmi na Abha FC ya Saudi Arabia Alhamisi”.
“Kocha Pitso atarejea dimbani na amesaini mkataba wa miezi minne na timu hadi mwisho wa msimu.
"Jukumu lake liko wazi na hiyo ni kuhakikisha Abha haishuki daraja na kucheza Ligi ya Kuu ya nchini humo msimu ujao."
Abha kwa sasa ipo kwenye hati hati ya kushuka daraja ikiwa nafasi ya 17 katika timu 18 kwenye Ligi ya Saudia na pointi 14 baada ya michezo 19 na imesaliwa na 11 msimu huu. Kocha huyo amekuwa akihusishwa na klabu mbalimbali Afrika ikiwamo Zamalek ya Misri, Kaizer Chiefs na timu ya taifa ya Nigeria.