Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moses Phiri njia panda kuivaa KMC FC

Majeruhi Moses Straika wa Simba SC, Moses Phiri

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Moses Phiri huenda akaukosa mchezo wa Mzunguuko wa 18 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC FC utakaopigwa Jumatatu (Desemba 26).

Simba SC itakua mgeni wa mchezo huo utakaounguruma Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza majira ya saa Kumi jioni, huku ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Kagera Sugar juzi Jumatano (Desemba 21), mjini Bukoba.

Phiri yupo shakani kuukosa mchezo huo, kufuatia maumivu wa Mguu kuendelea kumsumbua, na kwa sasa Mshambuliaji huyo anatembea kwa usaidizi wa Magongo.

Leo Ijumaa (Desemba 23), Phiri alitarajiwa kufanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa jeraha linalomkabili, kufuatia rafu aliyochezewa na Beki wa Kagera Sugar Deus Bukenya.

Hata hivyo Klabu ya Simba SC haijatoa taarifa zozote kuhusu mpango wa Mshambuliaji huyo kufanyiwa vipimo huko jijini Mwanza, lakini ni dhahir taarifa rasmi itatangazwa.

Hadi sasa Moses Phiri ameshaifungia Simba SC mabao 10 katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara akitanguliwa na Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Mayele aliyefunga mabao 13.

Chanzo: dar24.com