Wed, 31 May 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Baada ya taarifa kusambaa kuwa Straika Mzambia Moses Phiri, anataka kuondoka Klabuni hapo kutokana na kukosa nafasi ya kuanza mara kwa mara.
Hivi sasa upepo umebadilika na Staa huyo ataendelea kusalia katika klabu ya Simba SC.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’ alimwita Phiri na kumweleza bado wanamhitaji, hivyo wakakubaliana kwa amani na sasa staa huyo bado yupo Simba.
“Uongozi umemwomba Kocha Robertinho kukaa nae kama ilivyokuwa kwa Clatous Chama na lengo ni kuona tunaendelea kumuona hapa Msimbazi,” kimesema chanzo kutoka klabuni Simba
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: