Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison utawaua

Bm+3+pic Morrison utawaua

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

KASI na ubora wa staa mpya wa Simba ndani ya mechi mbili imewatia matumbo joto wanaofuata kucheza na timu hiyo wakiwemo Yanga wenyewe ambao, wamekuwa wakimkejekeli kwenye mitandao.

Mghana huyo amekuwa kipenzi na gumzo midomoni mwa Wanasimba ingawa Yanga wamekomaa kwamba, ni mali yao na wameendelea kumshikilia kwenye usajili wao huku wakisisitiza anauzwa kwa Sh600milioni.

Morrison ameichezea timu hiyo michezo miwili wa kwanza wa Simba Day dhidi ya Vital’O ya Burundi dakika 45 za kipindi cha kwanza na kutolewa, kwenye Ngao ya Hisani dhidi ya Namungo alitumika dakika 67.

Ametumika kwa dakika 112 kwenye ubora wake, ambazo amehusika katika mabao manne ikiwa ni kufunga, akatoa pasi ya mwisho na akasababisha penati.

Iko hivi, mechi ya kwanza kucheza ilikuwa dhidi ya Vital’O ya Burundi alitupia dakika 43, baada ya kupokea pasi ya juu kutoka kwa kiungo, Mzambia Larry Bwalya.

Katika mechi hiyo hiyo dakika 46, alitoa pasi ya mwisho kwa nahodha wa Simba, John Bocco ambaye alifunga bao la pili.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz