Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison kuikosa Yanga

Fc73e216a34dace564ffb11db611cf96 Morrison kuikosa Yanga

Fri, 30 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WACHEZAJI, Bernard Morrison wa Simba, Juma Nyosso wa Ruvu Shooting, Salum Kimenya wa Tanzania Prisons na Daruwesh Saliboko wa Polisi Tanzania wamefungiwa mechi tatu wakati mwamuzi Shomari Lawi akifungiwa kwa mwaka mmoja.

Hyao ni kwa mujibu taarifa iliyotolewa jana na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kilichokaa Oktoba 27 kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi.

Taarifa hiyo ilisema katika mchezo wa Tanzania Prisons dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, mchezaji wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya ametozwa faini ya Sh.500, 000 na kufungiwa michezo mitatu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Simba, Benard Morrison.

Aidha, ilisema katika mchezo namba 34 kati ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting, mchezaji wa Simba, Bernard Morrison ametozwa faini ya Sh 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Ruvu Shooting Juma Nyoso.

Kwa adhabu hiyo Morrison atakosa mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaochezwa Novemba 7.

Mchezaji wa PolisiTanzania FC, Daruwesh Saliboko ametozwa faini ya Sh 500,000 na kufungiwa michezo mitatu baada ya kutolewa kwenye mchezo kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa timu pinzani.

Pia mwamuzi Shomari Lawi ambaye alichezesha mchezo wa Tanzania Prisons dhidi ya Simba amefungiwa miezi 12 kwa kushindwa kuumudu mchezo huo aliochezwa Oktoba 22 kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa wakati mwamuzi Ramadhan Kayoko akikumbushwa kuongeza umakini katika majukumu yake.

Timu za Tanzania Prisons na Dodoma Jiji nazo zimepigwa faini ya Sh 500, 000 kila moja na Gwambina imetozwa faini ya Sh 3, 000,000 kwa kosa la kucheza dakika zote 90 bila ya kuvaa nembo ya mdhamini.

Mchezaji wa Ruvu Shooting, Shabani Msala ametozwa faini ya Sh 500, 000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga teke mchezaji wa Simba, Bernard Morrison.

Katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL), timu ya Majimaji FC imetozwa faini ya Sh 500, 000 kwa kosa la kuruhusu gari kuingia uwanjani na kuzunguka wakati mchezo ukiendelea, huku mashabiki wake wakiingia ndani ya uzio katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Chanzo: habarileo.co.tz