Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison atuliza presha Simba

Morrison Pic Data Morrison atuliza presha Simba

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author Mara. Bao pekee la kipindi cha kwanza la winga, Benard Morrison lilitosha kuipa ushindi Simba na kufikisha pointi 42, nne nyuma ya vinara wa Ligi Kuu, Yanga.

Simba, ambayo bado ina faida ya michezo miwili mkononi, ilikuwa na mchezo mgumu mbele ya Biashara United, ambayo ilikubai kipigo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Karume, mkoani Mara.

Akituliza pasi ndefu kutoka wingi ya kushoto, kiungo huyo raia wa Ghana, alituliza vizuri kabla ya kumchagua kipa wa Biashara dakika ya 21 na kufanya mchezo huo kuwa mgumu kwa wenyeji.

Kocha wa Simba Didier Gomes Da Rosa alimtumia Meddie Kagere katika eneo la ushambuliaji kama mshambuliaji pekee aliyekuwa akisaidiwa na Perfect Chikwende na Morrison kwa pembeni, huku katikati kukiwa na Mzamiru Yassin na Thedeo Lwanga.

kocha huyo pia aliamua kuwapumzisha Clatous Chama na Luis Miquessone, kabla ya kuamua kumwingiza kiungo fundi wa Zambia, Chama dakika za mwisho kutokana na kuumia kwa Morrison.

Mchezo huo ulikuwa muhimu kwa Simba kutokana na kutaka kusogea kileleni, lakini pia kuinua ari wakijiandaa na mchezo mgumu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz