Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison arejea kuwavaa Geita Gold

Morrison Hjk Morrison arejea kuwavaa Geita Gold

Sat, 29 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara baada ya kiungo wa kimataifa wa Yanga, Mghana, Bernard Morrison juzi Jumatano kumaliza adhabu yake ya kufungiwa michezo mitatu, ofisa habari wa timu hiyo, Ali Kamwe, ameweka wazi kwa balaa analolifanya nyota huyo kwenye mazoezi, wapinzani wao wajao wajiandae kisaikolojia, huku akitamba kuwa wataanza na Geita Gold leo.

Akizungumza na Championi Kamwe alisema: “Ushindi wetu dhidi ya KMC Jumatano ulikuwa muhimu hasa kutokana na presha kubwa ambayo bado wachezaji walikuwa wanacheza nayo mara baada ya kucheza michezo miwili iliyopita bila matokeo ya ushindi.

“Tuna mchezo muhimu na mgumu siku ya Jumamosi dhidi ya Geita Gold na kuelekea mchezo huu tunatarajia kiungo wetu Bernard Morrison atarejea kikosini baada ya kumaliza adhabu yake, ambapo katika kipindi chote alikuwa akifanya kazi kubwa mazoezini hivyo wapinzani wetu wajao wajiandae kisaikolojia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live