Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison apigwa chini FAR Rabat

Morrison Drs Morrison apigwa chini FAR Rabat

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka nchini Morocco zimeelezwa kuwa, Klabu ya FAR Rabat ya nchini humo imeamua kutomsajili fowadi wa Ghana, Bernard Morrison baada ya wiki kadhaa za majaribio katika klabu hiyo.

Morrison alifunga bao moja katika mechi ya kirafiki dhidi ya JSS. Sababu ya kutosajiliwa inadaiwa kuwa ni tabia zake.

Toto Tundu alikwenda FAR Rabat kufanya majaribio kwa muda wa wiki mbili baada ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ambaye kwa sasa yupo FAR Rabat kuhitaji huduma yake.

Mghana huyo alijiunga na Klabu ya Yanga katikati ya msimu wa 2019/20, akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na AS Vita Club ya Congo DR, lakini baada msimu huo kumalizika, alitimkia Simba ambako aliitumikia kwa miaka miwili kabla ya kurejea tena Yanga mwanzoni mwa msimu uliopita.

Morrioson amekuwa akisifika kwa kipaji kikubwa cha soka lakini jambo ambalo mara nyingi limekuwa likimponza ni tabia za utovu wa nidhamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live