Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison aongeza miaka miwili Yanga

99757 Pic+morson Morrison aongeza miaka miwili Yanga

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

MABOSI wa Yanga, wajanja sana, kwani baada ya kunusa za chinichini kwamba watani wao wanataka kuwazidi akili kwa Bernard Morrison, fasta wakaamua kufanya jambo moja la maana. Kupitia mmoja ya wadhamini wao, Kampuni ya GSM, Yanga imeamua kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wao huyo maarufu kama BM33, ili aendelee kukipiga Jangwani. Dili hilo limefanikiwa mchana huu kupitia kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Eng Hersi Said ambaye amekuwa bega kwa bega kuhakikisha klabu hiyo ikiwa na mafanikio msimu huu. Mkataba huo utamfanya Morrison aendelee kusalia katika kikosi hiko mpaka mwaka 2022 huku wakiwa wamefuta kabisa ndoto za watani wao Simba kumsajili baada ya kuibuka tetesi za chinichini kumuwinda. Mwanaspoti linafahamu kabisa kwamba matajiri hao tayari wana majina ya wachezaji wote ambao wanatakiwa kuongeza mkataba katika kikosi chao baada ya kufanyika maongezi ya kina na kocha wao Luc Eymael. Morrison alisaini mkataba wa miezi sita tu na kikosi hiko, lakini uwezo ambao ameuonyesha umewafanya matajiri hao washawishike kumuongezea mkataba. Sio Morrison tu, bali Yanga imeamua kukomaa na nahodha wake, Papy Kabamba Tshishimbi na wengine na utamu zaidi we nunua gazeti lako la Mwanaspoti kesho Jumamosi upate uhondo.

Chanzo: mwananchi.co.tz