Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison ana bahati ya mataji

Morrison Aziz Ki.jpeg Bernard Morrison

Thu, 11 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukisikia mastaa wenye nyota za bahati, huwezi kuacha kumtaja winga wa Yanga, Bernard Morrison mwenye kismati cha kuzichezea timu zinazokuwa kwenye upepo wa kunyakua mataji muhimu ya mashindano kama Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Kwa mara ya kwanza kuichezea Yanga mwaka 2020 aliitumika miezi sita kabla ya kuingia kwenye mgogoro wa kimkataba na viongozi na kutimkia Simba mwaka huo na kubeba mataji ya ASFC na Ligi Kuu akiwa na timu hiyo.

Alikaa Simba hadi msimu uliopita 2022 ambao timu hiyo ilishindwa kubeba taji lolote, ikiwa imetoka kutamba kwa kuchukua mataji mara nne mfululizo, kabla hajarudi Yanga msimu huu na hadi sasa ina uhakika wa kutwaa taji la Ligi Kuu Bara na imetinga nusu fainali mbili za ASFC na Kombe la Shirikisho Afrika na leo inacheza dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga inahitaji ushindi wa mechi moja tu kati ya tatu ilizobakiwa nazo dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya City na Dodoma Jii ili Morrison azidi kutamba na makombe huku akisubiri hatma ya timu hiyo kwenye michuano mingine ya ASFC na kimataifa na kudhihirisha bahati aliyonayo.

Ukiachana na Morrison, mwingine mwenye bahati ni aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Mbrazil Milton Nienov, ambaye msimu huu anainoa Yanga na anasubiria tu makombe yatue Jangwani, tofauti na mtalaamu wa misuli wa Simba, Fareed Cassem raia wa Afrika Kusini aliyewahi kuitumikia Yanga 2021 na sasa yupo Simba, hivyo amepishana na bahati ya mataji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live