Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison aiadhibu Simba, mbele ya Rais wa Tanzania na CAF

98386 YANGA+PIC Morrison aiadhibu Simba, mbele ya Rais wa Tanzania na CAF

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bao pekee la mshambuliaji Bernard Morrison limetosha kuipa Yanga ushindi muhimu dhidi ya watani zao jadi Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ushindi huo wa Yanga unaifanya kufikisha pointi 50 na kupanda nafasi ya tatu huku Simba ikibaki kileleni na pointi 68, huku Azam ikiwa nafasi pili na pointi 51. Morrison aliwainua mashabiki wa Yanga katika dakika 44, kwa kupiga mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Yanga. Bao hilo lilimfanya Rais John Magufuli kufurahi na kuwapungia mashabiki wa Yanga waliolipuka kwa shangwe kubwa baada ya bao hilo. Kiungo wa Simba, Clatous Chama alinusurika kupata kadi nyekundu katika dakika 33, baada ya kumkanya kwa makusudi kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, lakini mwamuzi Martin Saanya hakuona. Mshambuliaji Meddie Kagere nusura aifungie Simba bao baada ya shuti lake kugonga mwamba na kurudi uwanjani, naye Luis Miqussone alipiga shuti kali lililopanguliwa vizuri na kipa wa Yanga, Mechata Mnata. Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilitosha kuthibitisha jinsi Simba ilivyoingia kuwakabili wapinzani wao Yanga bila kujiamini. Yanga na Simba zinakutana kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara. Yanga ilianza mchezo huo kwa kasi na kuonekana kucheza kwa kujiamini, ikimiliki mpira, pasi nzuri na kasi  tofauti na Simba ambao wachezaji wake wengi walionekana kucheza taratibu. Wachezaji kama Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Clatous Chama, Francis Kahata walionekana kuwa na kasi ndogo tofauti na alivyozoeleka. Kutokana na Mkude, Chama kucheza taratibu na kuzidiwa katikati na Feisal Salum, Balama Mapinduzi na Haruna Niyonzima ilipelekea winga Luis Miquissone kati kuongeza nguvu. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.

Chanzo: mwananchi.co.tz