Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison: Young Africans ni zaidi ya Kaizer Chiefs

Image 604.png Morrison: Young Africans ni zaidi ya Kaizer Chiefs

Sat, 17 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Wakati Kocha kutoka nchini Tunisia Nasreddine Nabi akitarajiwa kutangazwa muda wowote kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, nyota wa zamani wa Ligi ya Afrika Kusini (PSL), Bernard Morrison amefanya ulinganisho kati ya Amakhosi na Young Africans, ambayo anaichezea kwa sasa.

Licha ya kupitia kipindi kigumu, Kaizer Chiefs imesalia kuwa miongoni mwa timu zinazofuatiliwa kwenye ligi ya Afrika Kusini. Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye vituko vingi nje ya uwanja, amesema Young Africans, ambayo ni bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la ASFC na wanafainali wa Kombe la Shirikisho Afrika ni wakubwa kuliko Kaizer Chiefs.

Morrison alikaa Afrika Kusini kwa miaka miwili akiichezea Orlando Pirates kabla ya kuondoka Julai 2018. Kisha alikwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa mwaka mmoja na baadae akatua Young Africans, Januari 2020, kabla ya kwenda Simba SC na kurejea tena.

“Hata Kaizer Chiefs inapokwenda kucheza ugenini haiwezi kuwa na mashabiki wengi kama ilivyo kwa Young Africans.”

“Namba za klabu (Young Africans) ni zaidi ya Kaizer Chiefs. Kwenda Kaizer Chiefs kunakuja na shinikizo lake,” amesema Morrison, ambaye alifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari cha Afrika Kusini.

“Lakini kama mchezaji, lazima uote kuchezea klabu kubwa maana yake ni lazima uwe tayari kwa kila jambo. Kama unahama kutoka Young Africans na kwenda Afrika Kusini kuchezea Kaizer Chiefs, lazima uwe tayari. Kwangu nadhani Presha kubwa ipo Tanzania kuliko Afrika Kusini.

“Hata Kaizer Chiefs wanapokwenda kucheza ugenini, hawapati umati huu mkubwa. Lakini hapa unapata namba kubwa kila wakati unapokwenda kwenye mechi. Lazima uwe tayari.”

Chini ya kocha ya Nabi, Young Africans imeshinda mataji sita katika misimu miwili, Ligi Kuu mara mbili, mawili ya Kombe la FA (ASFC) na Ngao ya Jamii mara mbili.

Chanzo: Dar24
Related Articles: