Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison: Sijaona mashabiki kama wa Tanzania duniani, ukifurahisha wanatoa fedha

99112 MORRISON1+PIC

Mon, 16 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

NDIYE Mghana pekee kwenye Ligi Kuu Bara, aliyeonyesha umahiri wa aina yake kwenye kutembea juu ya mpira. Mashabiki wa Yanga wanamkubali sana. Amewajengea heshima kubwa mbele ya watani zao wa jadi. Anaitwa Bernard Morrison ‘BM33’

“Huu ni ubora ambao nilijifunza kutoka kwa wachezaji wa zamani, unajua kila kitu unachofanya katika maisha unatakiwa uwashukuru waliokusaidia, hata hapa kuna watu wamenisaidia kujifunza.

“Balama Mapinduzi na Haruna Niyonzima kuna vitu najifunza kutoka kwao lakini inawezekana wapo ambao nao wanajifunza vitu kutoka kwa mtu mwingine au hata kwangu, kwahiyo wakati nikiwa Afrika Kusini kuna wachezaji wenzangu wawili walikuwa wazuri katika staili ya shibobo pale Orlando Pirates, nilijifunza kutoka kwao. Kila wakati wa mazoezi walikuwa wananifundisha.”

 Kocha na Shibobo?

“Namuelewa anachosema lakini sidhani kama anamaanisha kiuhalisia hilo, sioni kama naweza kuacha na ndio maana nimeendelea kufanya vile kuna wakati mashabiki lazima waburudike zaidi.

“Mashabiki wanalipa viingilio kuja kuangalia timu yao na inaposhinda ni vyema wakapata kitu tofauti cha kusimulia wenzao wanaporudi majumbani kwao napenda kuona watu wanaburudika na ndio maana soka pia ni burudani.

“Nawapenda sana mashabiki wa soka, kuna kitu nimekutana nacho hapa ni cha kipekee sana, mashabiki wamejaa uwanjani kuzishangilia timu zao lakini bado wanaona mchezaji amefanya vizuri wanampa pesa tena, hiki ni kitu tofauti sana nafikiri hili linamfanya kila mchezaji ajitume zaidi ili kuipa matokeo mazuri timu yetu na kuwafanya mashabiki wafurahi zaidi,” anasema Morrison.

“Tangu nimefika hapa nilihitaji kuzoea kidogo lakini nashukuru nimekutana na wenzangu ambao ilikuwa rahisi kupata ushirikiano na hiyo ndio familia ya soka inavyoishi.

“Wakati nafika nakumbuka mchezo wa kwanza niliukosa dhidi ya Azam niliumia kuona timu inapopoteza na mimi nashindwa kutoa mchango wangu, kilichoniuma zaidi ni kwa mba timu ilicheza vizuri siku hiyo lakini ikapoteza kwa bao moja niliumia baada ya hapo mambo yalianza kukaa sawa taratibu na sasa naona kuna mwanga mzuri unakuja,” anafafanua Morrison.

Nafasi nzuri?

Tangu amefika Yanga Morrison amekuwa akichezeshwa kiungo mshambuliaji akitokea pembeni na sasa anaelezea nafasi sahihi anayopenda kutumikia: “Mimi ni mshambuliaji tena mshambuliaji halisi namba tisa lakini sina tatizo ninapocheza kutokea kulia au hata kushoto au hata mshambuliaji wa pili itategemea wapi kocha anataka nicheze lakini nikicheza namba tisa huwa nakuwa huru zaidi.”

Mabao, asisti

“Soka ni lilelile kokote utakapo kwenda, kokote utakapokwenda ukipata uwanja mzuri ukichezea timu nzuri kila unachopanga kinaweza kutekel ezeka, unapocheza timu moja na watu kama Pappy (Tshishimbi), Feisal (Salum), Haruna (Niyonzima) pia ukiwa na Balama (Mapinduzi) hata yule Kaseke (Deus) wakiwa eneo la kati utagundua kabisa ubora wao, lazima utapata nafasi ya kufanya vitu vizuri.

 Miundombinu

“Kuna baadhi ya viwanja naona vina changamoto sana naona kabisa vinaathiri ubora wa soka la nchi hii, unapocheza katika Uwanja Mkubwa wa Taifa au hata ule wa Uhuru ni tofauti kabisa na ule Uwanja wa Singida au hata Tanga, ukicheza katika viwanja vya namna hiyo kuna uwezekano mkubwa ukakosa nafasi ya kuonyesha ubora wako, kuna haja viwanja vingine navyo vikaboreshwa.

Yanga na mataji?

“Ligi bado inaendelea hatujakata tamaa muhimu sasa ni kuendelea kushinda mechi zetu za ligi, nafahamu kwamba Simba inaongoza ligi kwa tofauti kubwa. Hatutakiwi kuangalia nini wanafanya tunapaswa kushinda mechi zetu, siwezi kutoa ahadi kwamba tuchukua taji lakini muhimu ni kuendelea kushinda, lakini kuhusu Kombe la FA hizi ni mechi za mtoano kila mchezo kwetu ni fainali.”

Asisti, kufunga?

“Kwangu kinachotangulia ni kutoa pasi ya bao hiki ni muhimu sana.  Huwa nikitoa pasi itakayozalisha bao najiona kama nimefunga. Kama hautaweza kutengeneza hautafunga kwa hiyo pale unapotengeneza ndiyo nafasi inapatikana, huwa napenda kuwatanguliza wachezaji wenzangu na timu kabla ya mafanikio yangu binafsi.”

 Simba wakoje?

“Mechi ilikuwa ngumu kama mlivyoona kila timu ilijipanga kuhakikisha inalinda heshima yake kwa ushindi, Simba ni timu ngumu naiheshimu lakini mwisho wa mchezo tulikuwa washindi, nilichojifunza katika mechi ile ni kwamba kila mchezaji hataki kuwaangusha mashabiki wa timu yake, presha inakuwa kubwa lakini binafsi nimecheza mechi kama zile nyingi kule Afrika Kusini dhidi ya Kaizer Chiefs.”

“Haikuwa rahisi kwangu kucheza ile mechi kwa kuwa nilikuwa naumwa lakini baadaye nikaona bora niombe hata dakika 45 tu za kucheza ili niisaidie timu yangu.”

 kiatu gani?

“Hapo kabla nilikuwa natumia kiatu aina ya Puma lakini baada ya kwenda Pirates nilianza kutumia Adidas, unajua pale vifaa vyao vyote mpaka mataulo ya kuogea wanatumia ya Adidas sasa nikaanza kutumia viatu hivyo na ndio natumia mpaka sasa.

alichoiulia Simba

“Kile kiatu nilichovaa katika mchezo wa Simba pia ni Adidas toleo jipya kabisa aliniletea mke wangu kama zawadi na siku ya kwanza kukivaa ilikuwa katika mchezo dhidi ya  Simba. Nashukuru kilinisaidia kufunga bao zuri na muhimu kwa timu yangu.

“Unajua najua kufunga kwa adhabu ndogo sina tatizo, ilikuwa kama kupata nafasi tu niliangalia jinsi kipa alivyokaa pamoja na wale mabeki waliokaa katika ukuta akili ikaja nifanye vile kwa kuwa naweza sikushangaa kuona nimefunga tena likawa bao zuri na muhimu kwa timu yangu.”

Alikujaje Yanga?

“Haikuwa rahisi, kabla ya kuja hapa nilikuwa na ofa kutoka klabu kama tatu na ofa nilizokuwa nazo Yanga ndio ilikuwa na dau la chini kuliko nyingine.

“Katika maisha kuna wakati unafanya maamuzi sio kwa kuangalia wingi wa fedha, unaangalia heshima tu ambayo unaweza kupewa na hiki ndicho kilichotokea kuja kwangu Yanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz