Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison, Nchimbi wako chini ya uangalizi

99574 Morrison+pic Morrison, Nchimbi wako chini ya uangalizi

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

MICHEZO yote imesimamishwa hapa nchini kutokana na agizo la Serikali ikiwa ni sehemu ya kupambana na virusi vya Corona ambavyo vimekuwa hatari zaidi kwa sasa duniani. Mpaka kufikia jana Jumatano mchana Tanzania ilikuwa imetangaza visa vitatu Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha.

Baada ya agizo hilo, Kocha wa Yanga, Luc Eymael amewapumzisha mastaa wake akiwemo Ditram Nchimbi, Bernard Morrison na wengineo lakini watakuwa chini uangalizi mkali na wamepewa maagizo mazito ambayo wasipoyatekeleza watakuwa kwenye wakati mgumu.

Ameliambia Mwanaspoti kuwa: “Kocha wa viungo Riedoh Berdien, amewapatia ratiba ya aina ya mazoezi wachezaji wote ambayo wanatakiwa kufanya kwa kipindi hiki wakiwa majumbani kwao, ratiba ya chakula ambacho wanatakiwa kula, ratiba ya kuishi kwa maana ya muda wa kufanya mazoezi na mambo mengine ya msingi.”

“Baada ya hapo tutakuwa tukiwasiliana kupitia video za WhatsApp, ili kuangalia maendeleo ya kila mchezaji kile ambacho anatakiwa kukifanya kwa wakati huu na kama itatokea kuna ambaye atafanya tofauti na hivyo tutagundua kwani anaweza kuongezeka uzito au kiwango chake kitapungua jambo ambalo anatakiwa kutupa maelezo ya kutosha kwa nini imekuwa hivyo,” alisema Eymael ambaye ameuambia uongozi hivi karibuni umtafutie David Molinga timu ya kucheza msimu ujao kwani ustaa wake umemchosha.

“Zoezi hilo la kumfuatilia kila mchezaji wakati huu hata mimi nitalifanya nikisaidiana na Berdien pamoja na mtaalamu wetu wa misuli ili kufahamu maendeleo ya kila mchezaji na ambacho anatakiwa kufanya mpaka pale ambapo tutakuja kukutana,” alisisitiza Eymael na kuongeza anataka wachezaji wake wawe fiti kwavile anajua wakirudi ratiba itakuwa ngumu na watakutana na robo fainali ya Kombe la FA.

“Wachezaji na benchi la ufundi kila mmoja anatakiwa huko alipo ajikinge na kuwa makini dhidi ya maambukizi haya ya ugonjwa wa Corona,”alisema Eymael ambaye mambo yakienda vizuri leo Alhamisi atakwenda kwao Ubelgiji ili kupata muda wa kupumzika na familia yake lakini msaidizi wake, Berdien nae atakwenda kwao Afrika Kusini.

Pia Soma

Advertisement

SIMBA NA UBINGWA

Simba ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kutokana na takwimu zilivyo lakini jana jioni uongozi wao ulikutana na kuangalia njia sahihi ya kuwalinda wachezaji wao kuhakikisha wanakuwa fiti ili wasitoke kwenye njia ya kombe ambalo Azam FC inalinyemelea.

Wekundu hao wa Msimbazi mbali na kujadili corona kwenye kikao hicho, lakini ishu nyingine ilikuwa ni kutumia kipindi hiki kifupi kufanya mawasiliano na vichwa kadhaa ambavyo wamepanga kuviongeza kwenye usajili mpya tayari kwa michuano ya kimataifa inayoanza Agosti mwaka huu kama CAF haitatoa maelekezo mapya.

Wachezaji wote wa Simba, wameambiwa watatumiwa utaratibu wa nini cha kufanya kupitia kwenye kundi lao la Whatsapp.

Wachezaji wa kikosi cha Simba mara baada ya kumaliza mazoezi jana Jumatano saa 5:00 asubuhi waliruhusiwa kuvunja kambi ya mazoezi.

Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mzingisa alisema wamewaita viongozi wote wa timu zao kwa maana ya Wanawake, Vijana na Kubwa walikuwa na kikao kizito jana jioni na watatoa muongozo.

AZAM WAMEWATOA

Thabit Zakaria Ofisa Habari wa Azam FC alisema kambi za timu zote kuanzia za vijana chini ya miaka ya umri wa 17 na 20 na wakubwa zote zimevunja.

“Wakubwa tunawaruhusu kila mmoja kwenda nyumbani kwake tutajua jinsi ya kuwasiliana kwa tatizo hili,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz