Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison, Mugalu wapewa siku sita

Mugaluu+pic Morrison, Mugalu wapewa siku sita

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MASTAA wa Simba wakiongozwa na Bernard Morrison, Chriss Mugalu na wenzao wengine wa kikosi cha Simba wamepewa siku sita ngumu ili kujifua na kuiva kabla ya kurejea kwenye mechi za Ligi Kuu, Kombe la ASFC na Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa na moto mkali.

Unaambiwa, kikosi cha Msimbazi kilichosalia nchini baada ya wenzao kadhaa kuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa, wataanza mazoezi kuanzia leo baada ya kuwa mapumzikoni kwa muda wa siku tano tangu walipoifumua Al Merrikh ya Sudan kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baadhi ya wachezaji watakaohusika na mazoezi hayo ya utimamu wa miili yao na kujengwa tayari kuibeba timu yao ni pamoja na; Ally Salim, Benno Kakolanya, David Kameta, Gadiel Michael, Ibrahim Ame, Bernard Morrison, Junior Lokosa, Pascal Wawa, Ibrahim Ajibu, Chriss Mugalu na wengineo.

Kocha wa Simba, Didier Gomes amewapa ratiba ya mazoezi ambayo wachezaji wake wanatakiwa kuifuata huku sehemu kubwa ya mazoezi yanaonekana kuwa yale ya nguvu.

Mwanaspoti liliinasa ratiba na sehemu kubwa ni mazoezi ya utimamu wa mwili kwa wachezaji wake ambayo kocha wa viungo, Mtunisia Adel Zrane ndio atakuwa akiwasimamia na inaonyesha leo saa 10:30 jioni ndio kina Morrison wataanza mazoezi mbalimbali ya viungo wakitumia vifaa mbalimbali, kukimbia mbio ndefu na fupi kucheza mpira na tizi nyingine za kuwaivisha.

Kesho Jumatatu mastaa hao watakuwa na awamu moja ya mazoezi ambayo watafanya asubuhi katika gym ambayo ipo ndani ya kambi yao Bunju na Zrane atakuwa akiwasimamia wachezaji wote 12, ambao waliobaki na hawakwenda katika majumu ya timu zao za taifa.

Jumanne kutakuwa hakuna kulala kwani wachezaji watakuwa na ratiba ya awamu mbili ya kufanya mazoezi asubuhi saa 3:00 watafanya uwanjani na watakwenda kupumzika kambini na kupata chakula cha mchana kisha saa 10:30 jioni watafanya awamu ya pili hapo hapo uwanjani.

Wachezaji wa Simba Jumatano watakuwa na awamu moja ya mazoezi ambayo yataanza kufanyika saa 10:30 jioni katika uwanja wao wa mazoezi Mo Bunju Arena.

Zrane ataendelea kusimamia tena shoo ya mazoezi siku ya alhamisi ambayo ratiba yao inaonyesha watakuwa na mazoezi ya gym kwa masaa mawili kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 5:30 asubuhi.

Ratiba hiyo itamalizika Ijumaa kwa wachezaji wa Simba kwa kufanya mazoezi kwa awamu mbili asubuhi saa 3:30 mpaka saa 5:00 kisha watakwenda kupumzika kambini kwao na kupata chakula cha mchana.

Wachezaji wakiwa wanasikilizia ratiba ya wiki ijayo watakwenda kufunga wiki kwa mazoezi ya uwanjani ambayo yataanza saa 10:30 jioni.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema ratiba yao ya mazoezi imeingiliana na msiba wa nchi ambao kipindi hichi ni wakati wa maombolezo kama nchi.

“Tunacheza mechi ya tano katika Ligi ya Mabingwa Afrika Aprili 2, dhidi ya AS Vita ya DR Congo, hivyo tutangalia namna gani ya kuweka ratiba yetu sawa kama matakwa ya nchi ambavyo yanahitaji,” alisema na kuongezea walipanga kuanza mazoezi leo Jumapili.

Simba inaongoza msimamo wa Kundi A ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa mbele ya Al Ahly ya Misri, AS Vita na Al Merrikh, lakini ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara nyuma ya Yanga inayoongoza kwa tofauti ya alama nne tu na pia ipo hatua ya 16 Bora ya ASFC.

Mechi ijayo

Ligi ya Mabingwa Afrika

Aprili 2, 2021

Simba vs AS Vita

Kombe la ASFC

Aprili 4, 2021

Simba vs Kagera Sugar

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz