Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison Mchezaji Bora Mwezi November

FFmX4aOXsAQT2N8 Benard Morisson akipokea tuzo yake

Thu, 2 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Bernard Morrison amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Novemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Kiungo huyo amewashinda mshambuliaji Medie Kagere na kiungo Jonas Mkude ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Novemba, Morrison amecheza jumla ya dakika ya 235 akifunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa magoli mengine mawili.

Bernard atakabidhiwa kitita cha Sh 2,000,000 kama sehemu ya zawadi kutoka kwa wadhamini wa tuzo hizo Kampuni ya Emirate Aluminium ACP.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa;

Bernard Morrison kura 2117 (46.77%)

Meddie Kagere kura 2115 (46.73%)

Jonas Mkude kura 294 (6.50%)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live