Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison, Bangala, Aziz Ki 'out' Yanga

Morrison Mcds.jfif Morrison, Bangala, Aziz Ki 'out' Yanga

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa kihistoria Yanga Sc, Cedric Kaze amesema kuwa wachezaji wanne wa timu hiyo wataukosa mchezo wao dhidi ya Ihefu hapo kesho.

Nyota hao wanne ni Azizi Ki raia wa BurkinaFaso, Bernard Morrison wa Ghana, Yanic Bangala wa DR Congo, Aboutwalib Mshery na Zawadi Mauya wa Tanzania kutokana na matatizo mbalimbali.

Inadaiwa kuwa Aziz Ki, Morrison na Bangala wamechelewa kujiunga na kambi huku Mauya akiwa majeruhi na Mshery amejitonesha jeraha.

Young Africans watashuka katika Dimba la Mkapa kesho huku wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Ihefu kwenye mechi iliyotibua Unbeaten 49 za Wananchi.

Kwenye mchezo huo uliyopigwa Highland Estate mkoani Mbeya Yanga SC ilikufa kwa bao 2-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live