Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morrison Agoma Kuandika Maelezo kwa CEO Barbara

Bernard Morrison Signs For Simba Sc Pea5nkp57riv1gjc4siy89exb Morrison Agoma Kuandika Maelezo kwa CEO Barbara

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HABARI kutoka kwa watu wa karibu wa nyota Benard Morrison  wamesema kuwa winga huyo amegoma kuandika maelezo kwenda kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba kuhusu tuhuma za kinidhamu anazotuhumiwa na klabu hiyo.

Morrison raia wa Ghana anadai kuwa yeye hana kosa hawezi kuandika maelezo yoyote wakati huo wazee wa klabu ya Simba SC wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuachana na Morrison haraka iwezekanavyo.

Aidha, Klabu ya Simba imethibitisha kutopokea barua ya maelezo kutoka kwa Morrison ambaye wamemsimamisha kwa makosa ya utovu wa nidhamu, Februari 4, 2022. ambapo klabu ya Simba ilitoa taarifa ya kumsimamisha mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa Ofisa wa idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema klabu bado haijapokea maelezo kutoka kwa mchezaji wao Bernard Morrison. Mchezaji huyo anapaswa kuandika barua ya maelezo kwenda kwa mtendaji mkuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live