Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morris: Soka kama unajua, unajua tu!

Aggrey Moris Aggrey Morris

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki na nahodha wa zamani wa Azam FC na Taifa Stars, Aggrey Morris ameviangalia vikosi vinavyochuana kwenye ligi mbalimbali nchini, kisha akatoa somo kwa wachezaji chipukizi akiwaambia lazima wakaze buti, ili kubadilisha ndoto zao ziwe kweli akisisitiza kwenye soka kama mtu anajua, anajua tu!

Morris alisema ni lazima wachezaji hao wazingatie mambo matatu yatakayofanikisha ndoto zao na kuepuka hisia za upendeleo.

Mkongwe huyo aliyegeukia ukocha kwa sasa na aliyewahi kuichezea Mafunzo msimu wa 2003 -2009 akitwaa nao mataji ya Ligi Kuu Zanzibar kabla ya kutua Azam 2009 -2023, aliliambia Mwanaspoti kuwa, soka halidanganyi, ili mchezaji aweze kufanikiwa lazima nidhamu ya kazi iwe sehemu ya maisha, kupenda kazi anayoifanya na bidii, haviwezi kumtupa.

“Ili kazi ya soka iwe rahisi kwa mchezaji anatakiwa kuwa na nidhamu na kuipenda kazi hiyo hakuna atakayemsukuma kufanya mazoezi, kulala kwa wakati, kuongeza maarifa ya kazi yake kwa kujifunza kwa watu mbalimbali duniani, hivyo vitu lazima vitamfanya ajitofautishe na wengine,” alisema na kuongeza;

“Hakuna njia ya mkato kwenye maisha nje na bidii na ndoto za wachezaji wengi nikufika mbali, vipaji vyao viwalipe, inawezekana kwani soka halina upendeleo zaidi ya kuzingatia masharti yake.”

Alisema mbali na wanasoka watu wengi wana ndoto, ila changamoto inakuja kuzibadilisha kuziishi kwenye uhalisi, kwani wengi wao maisha yao ni tofauti na kile wanachokiwaza.

“Mwenye kutimiza ndoto ni mwenye ndoto mwenyewe, hakuna mtu atazitoa kwenye kichwa na kuanza kuzifanyia kazi kama mhusika hataweka nguvu za kuzipambania ili kuzitafsiri kwa matendo, hivyo kazi yoyote inatakiwa utayari na kujitoa,” amesema mkongwe huyo.-

Chanzo: Mwanaspoti